Waziri Mkuu afuturu na watoto wenye mahitaji maalum

0
243

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka Wazazi na Walezi nchini wenye tabia ya kuwaficha watoto  wenye ulemavu kuacha kufanya hivyo, na badala yake wahakikishe wanawapa fursa ya kupata elimu.

Waziri Mkuu ameyasema hayo alipofuturu na watoto wenye mahitaji maalum wa kituo cha Buigiri wilayani Chamwino mkoani Dodoma ambacho kinamilikiwa na Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika.

Amesema ili kuhakikisha watoto wenye Ulemavu wanapata elimu, Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia mahitaji mbalimbali kwa ajili ya kujifunza na kufundishia.
 
Naye Askofu wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika Dkt. Dickson Chilongani amemshukuru Waziri Mkuu Majaliwa kwa kitendo chake cha kula futari na watoto wenye mahitaji maalum.

Amemuhakikishia Waziri Mkuu kuwa kanisa hilo litaendelea kuiunga mkono Serikali katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo pamoja na kudumisha amani.