Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo amekutana na kuzungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, Dar es Salaam.
Awali, mkutano kati ya Waziri Mkuu na Kamati ya Wafanyabiashara hao, watendaji wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na mawaziri wa sekta husika ulipangwa kufanyika Jumatano Mei 17, 2023 Magogoni, Dar es Salaam kwa uratibu wa Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla.
Waziri Mkuu amekutana na wafanyabiashara hao kutokana na umuhimu wa suala lililokuwepo, ambapo wafanyabiashara hao wa Soko Kuu la Kariakoo wametangaza kuanza mgomo kwa kufunga maduka yao hadi hapo madai yao yatakaposikilizwa na kupatiwa ufumbuzi.