Waziri Mhagama: NEC haitokwama kutimiza majukumu yake

0
298

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, kazi, Ajira ,Vijana na watu Wenye Ulemavu Jenista Mhagama amewatoa hofu watanzania na kusema kuwa uchaguzi utakaofanyika mwezi Oktoba mwaka huu utakuwa huru na wa haki.
 
Akizungumza Jijini DSM wakati akipokea magari 12 yaliyonunuliwa na Tume ya Uchaguzi NEC kwa ajili ya maandaalizi ya uchaguzi huo Mhagama amesema Serikali itahakikisha NEC haikwami katika kutimiza majukumu yake. 
 
Kwa upande wake Mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage amesema maandalizi ya uboreshaji wa daftari la kudumu awamu ya pili yanaendelea vizuri, magari hayo ni Kati ya ishirini yanayotarajiwa kununuliwa na NEC