Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi, amekabidhi rasmi eneo lenye ukubwa wa ekari 715 kwa halmashauri ya manispaa ya Kigamboni iliyopo mkoani Dar es salaam.
Waziri Lukuvi amekabidhi eneo hilo kufuatia agizo la Rais John Magufuli alilolitoa wiki iliyopita wakati wa uzinduzi rasmi wa wilaya ya Kigamboni.