Waziri Lugola azitaka kampuni za ulinzi kujiimarisha

0
468

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, – Kangi Lugola amesema kuwa, serikali itazifuta Kampuni za ulinzi binafsi nchini, ambazo zimekua zikiajiri askari vikongwe pamoja na wale wasiokuwa na mafunzo ya askari wa akiba yani Mgambo wala Jeshi la Kujenga Taifa – JKT. 

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo mkoani Mara, wakati akizungumza katika mkutano wa hadhara na wakazi wa jimbo la Mwibara wilayani Bunda.

Amesema kuwa baadhi ya kampuni hizo za ulinzi za binafsi, zimekua zikivunja sheria kwa kuajiri walinzi wasiokuwa na mafunzo, askari waliostaafu ambao wamechoka na zimekua zikiwalipa walinzi hao mishahara midogo ama kutowalipa kabisa.