Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro Edward Mpogolo, kumsaka mkandarasi kutoka kampuni ya Njarita anayesambaza umeme katika vijiji vya Same kutokana na kutokuwepo katika eneo lake la kazi kwa muda mrefu licha ya kulipwa fedha na serikali.
Dkt. Kalemani ametoa kauli hiyo wakati akizindua mradi wa ujazilizi wa usambazaji umeme vijijini, fungu la pili kwa mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika katika kijiji cha Mheza kata ya Maore wilayani Same.
Waziri huyo ameagiza pia mkandarasi huyo kusakwa na kuhojiwa kwanini amekataa wito wa Waziri kufika katika tukio hilo.
Dkt. Kalemani amesema mkandarasi huyo amesimamisha nguzo katika makazi ya watu ambazo hazina umeme na wananchi hawajaunganishiwa umeme mpaka sasa.
Sauda Shimbo, Kilimanjaro