Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa –TAMISEMI, Selemani Jafo amewaagiza wataalamu wa Idara ya Elimu TAMISEMI kutathmini sababu ya baadhi ya shule za mkoa wa Mara kufanya vibaya katika matokeo ya kidato cha sita.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo mkoani Dodoma ikiwa ni siku moja baada ya Baraza la Mitihani la Taifa -NECTA kutangaza matokeo hayo, huku akizipongeza shule za serikali zilizofanya vizuri katika matokeo hayo.
Katika mkutano na watendaji wa Idara ya Elimu -TAMISEMI Waziri Jafo amesema kati ya shule 100 bora 52 ni shule za kata.