Waziri Bashungwa ateta na Waandishi wa habari

0
224

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa, amewataka Waandishi wa habari nchini kuwa Wazalendo na kuandika habari zenye maslahi kwa Taifa.

Waziri Bashungwa ameyasema hayo jijini Dar es salaam alipofanya mkutano na Waandishi wa habari.                 

Wakati wa mkutano huo Waziri Bashungwa amesema kuwa, kuna umuhimu wa kuwepo kwa maridhiano baina ya Wamiliki wa vyombo vya habari na Waandishi wao.

Waziri Bashungwa pia ameahidi kukutana na Wadau wa vyombo vya habari wakiwemo Wamiliki, kwa lengo la kutatua kero mbalimbali zinazojitokeza katika tasnia ya habari.