Waziri Aweso awapa somo maafisa ugavi

Ziara Mwanza

0
203

Waziri wa Maji Jumaa Aweso amewaagiza maafisa ununuzi na ugavi wa taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara hiyo kuachana na michakato inayochelewesha utekelezaji wa miradi ya maji, na badala yake watumie elimu waliyonayo kuharakisha miradi hiyo bila ya kukiuka sheria na kanuni za manunuzi.

Waziri Aweso ametoa agizo hilo mkoani Mwanza wakati wa mkutano wa maafisa ununuzi na ugavi wapatao 120 kutoka taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara ya Maji.

Pia amewataka maafisa hao kushirikiana na kutokuwa kikwazo cha utekelezaji wa miradi ya maji nchini.

Kwa mujibu wa Waziri Aweso, ni muhimu kwa maafisa hao wa ununuzi na ugavi wa taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara ya Maji wakashirikiana na wakashirikishana taarifa mbalimbali za manunuzi kwani kitengo chao ni miongoni mwa vitengo muhimu ndani ya wizara ya Maji.