Tuju apata ajali akielekea kwenye mazishi ya Moi

0
395

Katibu Mkuu wa chama cha Jubilee cha nchini Kenya, Raphael Tuju amekimbizwa hospitalini, baada ya kupata ajali eneo la Magina katika Barabara ya Nairobi-Nakuru, wakati akielekea kwenye mazishi ya Rais Mstaafu wa nchi hiyo Daniel Arap Moi.

Kufuatia ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Prado na teksi, Tuju pamoja na dereva wake walikimbizwa katika hospitali ya Kijabe kwa ajili kupatiwa matibabu ya awali.

Habari zaidi kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa, taratibu za kuwapeleka majeruhi hao jijini Nairobi kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi unaendelea.

Mara baada ya ajali hiyo Tuju ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Jubilee alilalamika kuwa na maumivu ya kifua, huku dereva wake akiwa amevunjika mkono.

Mazishi ya Rais Mstaafu Moi aliyefariki dunia Februari 4 mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95 yanaendelea nyumbani kwake Kabarak mkoa wa Rift Valley.