Waumini wa dini ya Kiislamu wapongezwa kwa kumaliza mfungo

0
159

Rais John Magufuli amewapongeza Waumini wa dini ya Kiislamu nchini kwa kumaliza mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani, na amewashukuru kwa namna walivyoshiriki kuliombea Taifa hasa  katika kipindi hiki cha mapambano dhidi ya virusi vya corona.

Salamu hizo za  Rais Magufuli zimetolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya kumaliza kuswali sala ya Eid El Fitri katika Msikiti wa Gaddafi jijini Dodoma.

Waziri Mkuu Majaliwa pia amewasihi Watanzania wote kuendelea kushirikiana katika kulifanya Taifa liwe la amani na utulivu na kuwataka kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa corona.

Kwa upande wake Sheikh wa mkoa wa Dodoma, – Mustafa Rajab amempongeza Rais Magufuli kwa kuwapa Watanzania moyo wa kishujaa na ujasiri kwa kuwataka wamwombe Mwenyezi Mungu ili aliepushe Taifa na janga la corona, mataifa mengine duniani yakikumbwa na taharuki.