Kesi tatu za Uhujumu Uchumi zinazowakabili wahasibu wawili na mtunza kumbukumbu mmoja wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mtwara imeanza kusikilizwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara kwa kusikilizwa hoja za awali.
Baada ya kusikilizwa lwa hoja hizo za awali, kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 14,2024 na washtakiwa wote watatu wamerudishwa rumande.
Wanaoshitakiwa kwenye kesi hiyo ni Beda Nyasira na Theodosia Mtelani ambao ni wahasibu pamoja na Mahafudhi Chinenda, mtunza kumbukumbu.
Wanadaiwa kutenda kosa hilo mwaka 2023 baada ya kufanya malipo ya fedha za mirathi na kujinufaisha wao wenyewe kinyume cha sheria.