Watumishi wa afya waliolumbana wasimamishwa

0
153

Watumishi wawili wa afya wa Zahanati ya Ishihimulwa, Rose Shirima na James Getogo waliohusika kwenye video ya mabishano iliyosambaa mitandaoni wamesimamishwa kazi kwa muda ili kupisha uchunguzi.

Watumishi hao wamesimamishwa kazi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Uyui, Tabora, Dkt. Kija Maige ambaye amesisitiza kuwa wanapisha uchunguzi kwa mujibu wa kanuni ya 37 ya kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003.

Taarifa ya Halmashauri ya wilaya ya Uyui imeeleza kuwa “uchunguzi huo utashirikisha mabaraza yao ya kitaalamu ambayo ni Baraza la Wauguzi Tanzania na Baraza la Wataalamu wa Maabara Tanzania na hatua zaidi zitafuata baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.”

Waziri wa Afya, ummymwalimu ameandika katika ukurasa wake wa Instagram kuwa Tanzania ina akiba ya vifaa tiba na vitendanishi vya kupima malaria vinavyotosheleza kwa miezi sita ijayo.