Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) kamishna wa Polisi Salum Hamduni, amewataka Watumishi wa umma kote nchini kuzingatia miiko na maadili ya taaluma zao ili kuepuka kujiingiza katika vitendo vya rushwa.
Akizungumza na Watumishi wa hospitali ya wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma, Kamishna Hamduni amesema kila kazi ina miiko na maadili yake, hivyo ni muhimu kwa kila mtumishi kuzingatia.
Akiwa wilayani Kakonko Mkurugenzi Mkuu huyo wa TAKUKURU ameshiriki zoezi la upandaji miti katika haspitali ya wilaya hiyo, kuzungumza na Viongozi wa Watumishi katika idara mbalimbali, pamoja na kusikiliza kero za Wananchi.
Kamishna Hamduni yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya kikazi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Utumishi wa Umma.