Watumishi 4,000 warejeshwa kazini

0
370

Serikali imesema imewarejesha kazini na kuendelea kuwalipa mishahara jumla ya watumishi 4,380 walioondolewa kwenye orodha ya malipo ya mishahara kimakosa wakati wa zoezi la uhakiki wa vyetu vya elimu na watumishi hewa kote hapa nchini.

Kauli hiyo ya serikali imetolewa  na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deogratius Ndejembi bungeni jijini Dodoma na kusema idadi hiyo inajumuisha watendaji wa kata watendaji wa vijiji na watendaji wa mitaa wapatao 3,114.