Watumieni kwa faida vijana wataalamu

0
182

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi amewataka viongozi wa serikali za mitaa kote nchini kuwatumia vijana wataalamu kwenye maeneo yao.

Amesema hayo katika mkutano wa hadhara wilayani Manyoni Mkoa wa Singida.

Amewataka viongozi hao pia kuzingatia makundi ya vijana wasomi wa fani mbalimbali katika mchakato wa mikopo ya fedha kwa wanawake, vijana na makundi maalumu.