Jeshi la polisi mkoani Arusha limewakamata watuhumiwa 14 wa wizi wa pikipiki maarufu “Tatu Mzuka”, katika operesheni inayoendelea mkoani humo ya kupambana na wezi wa pikipiki.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Arusha Justine Masejo amesema kuwa, watuhumiwa hao wamekamatwa kwa tuhuma za kujihusisha na matukio mbalimbali katika jiji la Arusha, ikiwa ni pamoja wizi wa pikipiki na uporaji kwa kutumia pikipiki hizo.
Amesema mbali na kukamatwa kwa watuhumiwa hao 14, pikipiki 12 nazo zimekamatwa huku mbili kati ya hizo zikiwa hazina namba za usajili.
Kwa mujibu wa kamanda Maseja, watuhumiwa hao wamekiri kujihusisha na matukio ya uporaji.