Watuhumiwa wa ujambazi wauawa Kigoma

0
1193

Watu wanane wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na askari wa Jeshi la polisi mkoani Kigoma kwenye pori la Muyovozi wilayani Kakonko.

 Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kigoma, – Martin Ottieno amesema kuwa jeshi hilo lilipata taarifa kutoka kwa Wakazi wa kijiji cha  Mganza kuhusu uwepo wa vibarua wa mashambani wanaowatilia mashaka na walipokua wakiwafuatilia ndipo watu hao walipoanza kurusha risasi.

Kamanda Ottieno  ameongeza kuwa katika tukio hilo, mbali na kuuawa kwa watuhumiwa hao wa ujambazi, polisi pia wamekamata bunduki moja aina ya AK 47 ikiwa na risasi Kumi.