Watuhumiwa wa mauaji Itigi wafikishwa mahakamani

0
1176

Kesi ya mauaji inayomkabili Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Itigi mkoani Singida, -Pius Luhende na watu wengine Sita imetajwa leo kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi mkoa wa Singida.

Hii ni mara ya pili kwa watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani, ambapo kwa mara ya kwanza ilikua ni Februari 11 mwaka huu.

Waliofikishwa mahakamani hapo pamoja na Luhende ni Rodney Elias ambaye ni askari wanyamapori wa halmashauri ya Itigi, Makoye Steven ambaye ni askari wa wanyamapori hifadhi ya Doloto wilayani Manyoni, Mwanasheria wa halmashauri ya Itigi, – Eric Paul, Afisa Tarafa ya Itigi, – Eliutha Augustino, Afisa Kilimo na Mifugo wa halmashuari hiyo  Silvanus Lungwisha na Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kazikazi Yusuph John.

Mkurugenzi Mtendaji huyo wa halmashauri ya wilaya ya Itigi, -Pius Luhende na watu wengine hao Sita wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya Mkulima Isack Petro mkazi wa kijiji cha Kazikazi aliyeuawa kwa kupigwa risasi kanisani Februari Pili mwaka huu. 

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 11 mwaka huu.