Watu milioni 22 wahesabiwa sensa

0
179

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt. Albina Chuwa amesema hadi kufikia Agosti 25, kaya 5,060,158 zenye watu 22,004,910
zilikuwa zimekwishahesabiwa nchi nzima katika sensa ya watu na makazi inayoendelea nchini kote.

Amesema kati ya watu hao ambao tayari wamehesabiwa wanawake ni 11,413,045 (51.9%) na wanaume ni 10,591,865 (48.1%).

“Uchambuzi unaonesha kuwa mikoa yote 36 imeweza kuhesabu watu kwa wastani wa asilimia 36.8, mkoa unaoongoza kwa kasi kubwa ni Kaskazini Unguja ambapo asilimia 49.7 ya kaya zote zimeshahesabiwa.” amesema Mtakwimu Mkuu wa Serikali

Dkt. Albina Chuwa alikuwa akitoa takwimu hizo mkoani Dar es Salaam wakati wa kikao kilichoitishwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu aliitisha kikao hicho kwa lengo la kuzungumza na wakuu wa mikoa, kikao alichokiendesha kwa njia ya mtandao akiwa ofisini kwake Magogoni ambapo amewaagiza kusimamia kikamilifu zoezi la sensa.