Watu kadhaa wajeruhiwa ajali ya basi la Happy Nation

0
200

Baadhi ya abiria waliojeruhiwa katika ajali ya basi la Happy Nation iliyotokea usiku wa kuamkia leo mkoani Pwani,  wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Tumbi wilayani Kibaha.

Basi hilo lililokuwa na abiria zaidi ya 50, lilikuwa likisafiri kutoka mkoani Kagera kwenda Dar es Salaam.

Mkuu wa mkoa wa Pwani, Abubakari  Kunenge amesema ajali hiyo imetokea majira ya saa nane na nusu usiku kuamkia hii leo katika eneo la Vigwaza wilayani Bagamoyo.

Amesema baada ya ajali hiyo  majeruhi wengi walikimbizwa katika kituo cha Afya Mlandizi na  baadaye majeruhi tisa walihamishiwa katika hospitali ya rufaa ya Tumbi.