Watoto wanaozurula muda wa masomo kukamatwa

0
201

Mkuu wa mkoa wa Katavi, Mwanamvua Mrindoko ameziagiza halmashauri zote za mkoa huo kuanzisha oparesheni ya kuwakamata watoto wanaozurura muda wa masomo.

Mrindoko ametoa agizo hilo baada ya kufanikiwa kwa operesheni ya aina hiyo iliyofanyika katika halmashauri ya manispaa ya Mpanda.

Akitoa agizo hilo Mkuu huyo wa mkoa wa Katavi amesema suala la watoto kuzurula mitaani muda wa masomo halikubaliki, na kwamba wazazi ama walezi wa watoto watakaobainika kufanya biashara muda wa masomo watachukuliwa hatua.