Wafanyabishara wawili akiwemo mfanyakazi wa ndani ambao ni wakazi wa Kigamboni wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashitaka mawili ya kusafirisha dawa za kulevya aina ya HEROIN Kilogramu 882.71 na Methamphetamine Kilogramu 2167.29.
Wakili Mwandimizi wa Serikali HEMED HALFAN mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo AARON LYAMUYA amedai kuwa washitakiwa hao walikamatwa Desemba 12 mwaka huu wakisafirisha dawa hizo eneo la KIGUGUMO SHULE Wilayani KIGAMBONI.
Kesi hiyo namba 53 ya mwaka 2023 itatajwa tena Januari 11 mwaka 2024.
Waliopandishwa kizimbani ni Wafanyabiashara NAJIM ABDALLAH MOHAMED, MARYAM NAJIM MOHAMED na mfanyakazi wa ndani JUMA MBWANA ABBAS.