Watatu wafa maji Geita

0
251

Wavuvi watatu wamekufa maji baada ya mtumbwi wao kuingiza maji na kuzama katika Ziwa Victoria eneo la Mwalo wa Nungwe halmashauri ya wilaya ya Geita.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Geita, Cornel Magembe amefika katika eneo la tukio na kutoa rai kwa wavuvi kuvaa vifaa vya kujiokoa wanapokuwa ziwani katika shughuli zao za uvuvi.

‘Hakuna anayejua kuogelea pindi dharura inapotokea, ninawasihi sana wavuvi maji hayana mazoea tafadhalini mvae vifaa vya kujiokoa”. Amesema Magembe

Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nungwe, Elikana Ncheye amethibitisha taarifa za kuwepo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa tayari wameopoa miili ya wavuvi wawili kati ya watatu waliokufa maji.