Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge amesema watanzania wanatakiwa kuwa wazalendo kwa miradi ya taifa inayochochea maendeo.
Mbuge ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bwalo la uzalishaji mali kikosi cha 601 Kambi ya Ngerengere, ambalo limefanyiwa uakarabati mkubwa.
Jenerali Mbuge amebainisha kuwa ni vyema watanzania pia kutambua kazi inayofanywa na Jeshi la kujenga Taifa, ni kwa ajili ya wananchi wote hivyo kuwataka kulipenda nakushirikiana nao katika kuimarisha uchumi wa taifa lao.
” Ni jukumu letu sote kujenga nchi yetu kwa kufanya kazi za uzalishaji mali kwa uadilifu mkubwa ili kuleta matokeo chanya katika uchumi wake.”- Amesema Meja Jenerali Mbuge.
Katika kuunga juhudi za mwanzilishi wa Bwalo hilo, Jenerali Mbuge amemkabidhi Mkuu wa kikosi Namba 601, Kanali Zeno Sikukuu amesema jumla ya shilingi Milioni kumi zilitolewa na SUMA JKT kwa ajili ujenzi wa jengo jipya linalolenga kutoa huduma za kijamii huku akiwataka wakazi wa eneo hilo na wasafiri wanaotumia barabara ya Morogoro kwenda mikoani kutumia eneo hilo kwa mapumziko.
Aidha amewataka maafisa wa Jeshi kuwa wamoja nakuendeleza kazi iliyoasisiwa na Brigedia Jenerali Mohamed Mohamed ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia iendelee kunufaisha Jeshi na jamii inayowazunguka.
Baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamesema kuzunduliwa bwalo hilo kutaimarisha usalama wa raia na mali zao sambamba na kupatikana kwa fursa za ajira.