Watanzania watakiwa kutopotosha taarifa mbalimbali

0
385

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewaasa wanasiasa nchini kutotumia mlipuko wa virusi vya Corona uliotokea nchini China na kuua watu zaidi ya Elfu moja na Mia nne kujipatia umaarufu wa kisiasa. 


Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo jijini Dodoma mara baada ya kushiriki swala ya Ijumaa katika msikiti wa Gaddafi.


Amesisitiza umuhimu kwa Watanzania wote kuliombea Taifa ili Mwenyezi Mungu aliepushe na maafa mbalimbali. Pia ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuitegemea Serikali katika kupata taarifa za mara kwa mara kuhusu masuala mbalimbali zikiwemo zile za mlipuko wa virusi hivyo vya Corona, nzige pamoja na mafuriko.

Amesema kazi inayofanywa na serikali kwa sasa ni kuhakikisha nchi inaendelea kuwa salama, ambapo ametumia fursa hiyo kuwaomba wananchi waendelee kumuomba Mwenyezi Mungu.


Kwa mujibu wa Waziri Mkuu Mjajaliwa, katika mji wa Wuhan ambako virusi hivyo vilianzia, wapo vijana 497 wa Kitanzania na wote wapo salama na kwamba Se