Watanzania wametakiwa kuwa wazalendo katika kuilinda amani ya nchi kwani heshima ya Taifa lolote lile haitokani na kujipendekeza kwa Taifa jingine bali.
Hayo yamesemwa na Mbunge wa Siha, Dkt. Godwin Mollel wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Moshi na kuongeza kuwa Watanzania wasikubali kudanganywa kwani amani iliyopo ni tunu na haipaswi kabisa itoweke.
Mollel amesema ni wakati sasa kwa Watanzania kumuunga mkono Rais Dkt. John Magufuli katika kuhakikisha amani ya nchi haitoweki.