Watanzania washerehekea miaka 60 ya Uhuru

0
226

Watanzania leo Desemba 9, 2021 wanaadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika, Uhuru uliopatikana Desemba 9 mwaka 1961.

Maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika Uwanja wa Uhuru mkoani Dar es Salaam, mahali ambapo Tanganyika ilisherehekea uhuru mwaka 1961 kwa mara ya kwanza. Mgeni rasmi katika maadhimisho haya ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Kauli mbiu ya Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru ni “Miaka 60 ya Uhuru, Tanzania Imara, Kazi Iendelee”.

Uzinduzi rasmi wa juma la maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru ulifanywa Desemba 2, mwaka huu jijini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wakati wa juma hilo la madhimisho ya miaka 60 ya Uhuru kulikuwa na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na mashindano ya insha kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, michezo kama mpira wa miguu, mpira wa kikapu, mpira wa wavu na riadha, na mashindano ya baiskeli.