Watanzania wamehimizwa kutumia sikukuu za Mwisho wa mwaka kujitoa kwa ajili ya watu wenye uhitaji kwenye jamii wakiwemo wagonjwa walioko hospitalini.
Rai hiyo imetolewa na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Game Shawers Limited Juma Rajabu, wakati alipotembelea Taasisi ya Tumaini la Maisha iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutoa msaada wa mahitaji mabalimbali ikiwemo vyakula kwa watoto wenye saratani wanaopatiwa matibabu katika Hospitali hiyo.
Mkurugenzi huyo amebainisha kuwa ndani ya jamii wapo wahitaji wa aina mbalimbali hivyo mtanzania anayeguswa na watu wenye uhitaji mahali popote ana wigo mpana wa kumrudishia Mungu shukurani kwa namna atakavyokuguswa.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Taasisi ya Tumaini la Maisha Mwalimu Leonard William amewashukuru wadau mbalimbali waliofika katika kituo hicho na kutoa msaada wa vyakula na mahitaji mengine katika taasisi hiyo nakubainisha kuwa milango iko wazi kwa watanzania wote watakaoguswa na watu wenye uhitaji.
Huduma zinazotolewa katika Taasisi ya Tumaini la maisha ni pamoja na haki ya kupata elimu kwa watoto pamoja na huduma za matibabu