IGP Sirro awaonya vijana waotumika kuchafua Taifa

0
530

Watanzania wametakiwa kuacha kutumiwa na watu wasiokuwa na nia njema kwa Taifa ili kusababisha machafuko na uvunjifu wa amani.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro wakati akizungumzia hali ya usalama nchini na kutoa tathmini ya uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 28, mwaka huu.

“Tumewakamata watuhumiwa katika maeneo mbalimbali ambapo visiwani Zanzibar tumekamata mabomu ya kienyeji yaliyokuwa yameandaliwa kulipua kwenye visima vya mafuta na ofisi ya ZEC, ila tuliwahi kuwadhibiti,” Sirro ameeleza.

Katika hatua nyingine Sirro amesema watuhumiwa 254 wanashikiliwa kwa makosa mbalimbali kuhusiana na Uchaguzi Mkuu.

Ametoa wito kwa viongozi wa siasa wanaosema wanatishiwa usalama wao kuripoti kwenye vyombo vya usalama na sio kukimbilia nje ya nchi.

“Nmejitahidi mara kadhaa kumwambia aliyekuwa mgombea urais kupitia [CHADEMA] Tundu Lisu, kutoa taarifa kwa jeshi la polisi. Lakini amekimbilia ubalozini na hakutaka kutupa taarifa ili sisi tufanyie kazi.”

Kuhusu hali ya amani mkoani Mtwara vyombo vya ulinzi na usalama vipo kazini na amewatahadharisha wale wote wanaotaka kujaribu kujiunga na makundi yanayotishia amani ya nchi kuwa sheria zitachukuliwa.