Watanzania wahimizwa kulinda miradi ya nishati

0
113

Watanzania wameshauriwa kuwa mstari wa mbele katika kulinda miradi mikubwa inayoanzishwa na serikali, ukiwemo ule wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani mkoani Tanga.

Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa kamati ya kudumu ya bunge ya Nishati na Madini Dastan Kitandula, wakati wa ziara ya mafunzo ya kamati ya Nishati na Madini ya Bunge la Uganda kwenye mradi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Tanzania hadi Zambia (TAZAMA).

Kitandula amsema eneo kubwa la bomba la kusafirisha mafuta kutoka Hoima hadi Tanga lipo Tanzania, hivyo ni vema kwa Watanzania kuulinda mradi huo kwa kutambua umuhimu wake.

Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Dkt. Peter Lokeseri, ndiye aliyewaongoza wajumbe wa kamati ya Nishati na Madini ya bunge la Uganda katika ziara hiyo ya kutembelea mradi wa bomba la kusafirisha mafuta la TAZAMA

“Tanzania wana uzoefu mkubwa katika usafirishaji wa mafuta kwa njia ya bomba kwenda nchi zingine, hivyo uzoefu walionao kwa miaka mingi sasa utatusadia kujifunza mambo mengi yatakayokuwa na tija kwenye mradi huu mwingine wa Hoima hadi Tanga, ” amesema Dkt. Lokeseri