Watanzania wahimizwa kuendelea kuchangia damu salama

Utalii wa ndani

0
222

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Nickson Simon ( Nikki wa Pili) amewataka vijana na wageni waliofika katika hifadhi ya msitu asilia Pugu Kazimzumbwi kuendelea kuhamasisha vijana wengi zaidi kuendelea kuchangia zoezi la damu salama ili kuokoa kizazi cha Sasa na baadae

Nikki amesema wilaya ya kisarawe haijapata taarifa ya vifo vilivyotokana na ukosefu wa damu kwa mwaka jana na kuwataka wanafunzi hao kuendelea kuwa mabalozi wa kuhamasisha watanzania wengi zaidi kuchangia damu salama nchini

Akizungumzia ujio wa wanafunzi hao Afisa Muhifadhi Wilaya ya Kisarawe Fredy Ndandika anasema Pugu Kazimzumbwi ni eneo tulivu na kuna vivutio vingi ambavyo ukiwa katika eneo hili unaweza kuchangia damu salama huku unashuhudia vivutio vilivyopo ikiwemo Bwawa la minaki na miti ya aina mbalimbali

Wanafunzi zaidi ya 150 wakiambatana na Miss Tanzania 2022, Halima Kopwe wamejitokeza kuchangia damu salama wakiwa ndani ya hifadhi ya msitu asilia Kazimzumbwi uliopo Kisarawe Mkoani Pwani