Watanzania hii leo wanaadhimisha miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika kuadhimisha siku hiyo, hakutakuwa na sherehe yoyote iliyopangwa kufanyika kwa ngazi ya Kitaifa, na badala yake Wananchi katika maeneo mbalimbali wanafanya shughuli za kijamii na zile za kujiletea maendeleo.
Serikali imesema kuwa Shilingi Milioni 988.9 zilizopangwa kutumika endapo sherehe hizo zingefanyika zimeokolewa, na zitatumika kwa ajili ya shughuli nyingine.
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa Aprili 26 mwaka 1964 na aliyekua Rais wa Tanganyika kwa wakati huo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na mwenzake wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume.