Watanzania tusikubali kugawanywa

0
284

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara Abdulrahman Kinana amesema Serikali haikatai kukosolewa wala kusahihishwa ila ingependa hayo yasifanywe katika ajenda zitakazowagawa Watanzania.

Kinana ameyasema hayo mkoani Dodoma wakati wa mkutano wake na wanachama wa CCM pamoja na wananchi mbalimbali leo Mei 5, 2024.

Amewataka Watanzania wasihadaike na ajenda inayodhamiria kuwagawa bali waendeleze mshikamano na kudumisha Muungano ambao kwa sasa umedumu kwa miaka 60.

Tupo Mbashara kupitia TBC1, TBC Taifa na mitandao ya kijamii kwa anwani ya TBConline.

TBCDigitalUpdates

ChamaChaMapinduzi