Watu watano wamefariki dunia na wengine 10 wamejeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyohusisha daladala na lori la mchanga katika eneo la Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema kuwa Jeshi hilo linaendelea na uchunguzi zaidi.
Aidha, akielezea chanzo cha ajali hiyo iliyotokea saa 10 alfajiri leo, Mambosasa amesema dereva wa daladala alipita wakati taa nyekundu (zinazomzuia kupita) zikiwa zimewaka.
Daladala hiyo hufanya safari zake kati ya Temeke na Muhimbili jijini Dar es Salaam.