Mkurugenzi wa Redio Uhai FM ya jijini Dar es salaam, – Charles Hilary amesema kuwa, kuna tofauti kubwa ya utangazaji wa redio wa sasa na wa zamani.
Charles amefafanua kuwa, utangazaji wa redio wa zamani ulikua ni wa utulivu, umakini na ulikua unafunza zaidi kuliko ule wa sasa.
Akizungumza katika mahojiano na TBC ikiwa leo ni maadhimisho ya siku ya Redio Duniani, Charles amesema kuwa utangazaji wa sasa unamnyima msikilizaji kupata kile anachohitaji.
Amewashauri watangazaji wa redio wa sasa kukubali kukoselewa na kujifunza kila mara, ili kuhakikisha chombo hicho cha redio Chenye nguvu kubwa katika kupashana habari kuendelea kuaminika.
Redio Uhai FM inamilikiwa na kampuni ya Azam Media Limited ambayo pia ni mmiliki wa Azam TV.