Wakuu wa mikoa pamoja na wakuu wa wilaya nchini wameshauriwa kutotumia vibaya sheria ya kuweka watu ndani saa 48, na badala yake wafuate taratibu pindi wanapotaka kutumia sheria hiyo.
Kauli hiyo imetolewa jijini Tanga na Kaimu Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Dkt. Gerald Ndaki alipokua akizungumza na Waandishi wa habari.
Amesema ni vizuri kila kiongozi akatambua mipaka ya majukumu yake, huku akiheshimu utu na mamlaka yake pasipo kuvunja taratibu za utumishi.
Aidha amesisitiza suala la usimamizi wa haki na amani katika maeneo yote nchini kupitia Wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama ngazi za mikoa na wilaya.