Watakaofanya ukatili kunyimwa dhamana

0
107

Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, imejipanga kuweka mkakati kwa wale wote wanaofanya ukatili kwa wanawake na watoto wasipate dhamana, ili kuzuia kufanya matukio mengine wakiwa uraiani.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo Mwanaid Khamis wakati akipokea taarifa ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida iliyowasilishwa na mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro.

Amesema mkakati huo utajikita na kuweka sheria ya kutokuwapatia dhamana watu ama mtu yeyote atakayefanya ukatili kwa wanawake na watoto nchini.