Wastaafu kuhakiki taarifa kwa alama za vidole

0
486

Serikali imesema Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) una mpango wa kuweka vifaa vya uhakiki vitakavyotumia alama za vidole kwenye ofisi za halmashauri ili kuhakikisha zoezi la uhakiki kwa Wastaafu linafanyika kwa urahisi.

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu) Patrobas Katambi ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali lililoulizwa na Mbunge Maimuna Pathan aliyetaka kufahamu kwa nini Serikali isifanye utaratibu wa kwenda kuhakiki Wastaafu kwenye wilaya zao kuliko ilivyo sasa kuhakikiwa mikoani.

Katambi amesema vifaa hivyo vitasaidia ambao hawatakuwa na uwezo wa kutumia njia ya kieletroniki iliyopo sasa kuweza kuhakiki taarifa zao kwa alama za vidole katika halmashauri hizo badala ya kusafiri umbali mrefu kwenda kuhakikiwa jambo litakalookoa muda na kupunguza gharama za usafiri.