Utangulizi
Marehemu Marin Hassan Marin alikuwa mfanyakazi wa Shirika la Utangazaji Tanzania hadi umauti ulipomfika tarehe 01/04/2020. Marehemu amefariki katika Hospitali ya Lugalo, jijini Dar es Salaam leo tarehe 01/04/2020.
Elimu
Marehemu alizaliwa tarehe 15/07/1972. Alihitimu elimu ya stashahada ya Uandishi wa Habari mwaka 2004.
Ajira
Marehemu aliajiriwa na iliyokuwa Taasisi ya Utangazaji Tanzania tarehe 01/05/2005 kama Mwandishi wa habari Daraja la II. Marehemu alipanda madaraja mbalimbali hadi kufikia katika cheo cha Mwandishi wa Habari Mwandamizi cheo alichokuwa nacho mpaka umauti ulipomfika.
Wengi wetu ndani na nje ya TBC tutamkumbuka marehemu Marin Hassan Marin kwa mema yake ikiwemo uchapa kazi wake, kujitolea na ushirikiano na wenzake. Amelitumikia Shirika la Utangazaji Tanzania kwa uaminifu na uadilifu mkubwa kwa kipindi chote miaka kumi na tano (15). Marehemu ameacha Mke na Watoto.
Kwa niaba ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) tupenda kutoa pole kwa mke wa marehemu, watoto, familia, ndugu, marafiki na majirani wafanyakazi wote wa Shirika la Utangazaji Tanzania kwa msiba mkubwa uliotupata.
Mwenyezi Mungu awape uvumilivu na nguvu ya kuhimili kishindo hiki kizito cha kufiwa na mpendwa wetu na aiweke roho ya marehemu Marin Hassan Marin mahali pema peponi.