Washiriki wa elimu kwa umma wakumbushwa kujiendeleza

0
138

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha, amewakumbusha waandaaji wa vipindi vya Televisheni, Redio na Mitandao ya Kijamii kuwa na Utamaduni wa kujiendeleza kimasomo kwenye sekta ya uhabarishaji kutokana na kasi ya Teknolojia.

Dkt. Rioba amesema kwa sasa jamii inatumia Sana mitandao ya kijamii ambapo waandaji hao wanaweza kutumia njia hizo kuwafikia watu wengi zaidi.

Pia amewasisitiza kutumia mitandao ya kijamii kupata elimu mpya zinazoweza kuwasaidia kuhabarisha umma kwa Teknolojia ya sasa badala kutegemea elimu waliyoipata wakiwa chuo pekee.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), yakishirikisha maofisa wa habari wa Wizara, Taasisi, Mashirika ya Umma, Idara na Halmashauri.