Wasanii Manyara watakiwa kujisajili

0
208

Naibu Waziri Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza amewataka wasanii wa Mkoa wa Manyara kuhakikisha wanajisajili kama ilivyoutaratibu kwani gharama za kujisajili siyo kubwa.

Naibu Waziri Shonza akiwa katika picha ya pamoja wasanii wa Manyara

Shonza ametoa wito huo Wilayani Babati alipofanya kikao na wadau wa sekta ya Filamu kwa lengo la kufahamu changamoto zao.

Aidha Shonza amewasihi wasanii vijana kuunda vikundi na kwenda kuomba mikopo ya mfuko wa maendeleo ya vijana unaosimamiwa na Halmashauri ili kujikwamua kiuchumi.

Naye Kaimu Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Kiagho Kilonzo amesisitiza kuwa ofisi yake ipo katika mchakato wa kuanzisha kanzi data ya wasanii wa filamu nchini hivyo ni vyema wajisajili kwani kuna fursa nyingi zinawapita wasanii sababu hawapo katika mfumo rasmi wa kuwapata kwa haraka.