Waomba kujengewa madaraja makubwa

0
225

Mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara kwenye baadhi ya maeneo, ambapo mkoani Morogoro zimesababisha kukatika kwa mawasilino ya barabara ya kutoka Morogoro mjini kwenda Kisaki
katika kijiji cha Kiseleke wilaya ya Morogoro Vijijini.

Wakazi wa kijiji hicho wanaojishuhulisha na kilimo cha mpunga wameiomba Serikali iwajengee madaraja makubwa katika barabara hiyo muhimu inayotumiwa na watu mbalimbali wakiwemo watalii wanaotembelea hifadhi ya Taifa ya Nyerere na kuongeza kuwa madaraja yalipo sasa yamekuwa yakisombwa na maji msimu wa mvua.

Aidha, watumiaji wa vyombo vya moto pia wamelalamikia bidhaa zao kuchelewa kufika Kisaki, kwani mawasiliano ya barabara hiyo yamekuwa yakikatika mara kwa mara wakati wa msimu wa mvua.