Watumishi Wanawake wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kutoka vituo vya makao makuu na Bandari ya Dar es Salaam wametoa msaada wenye thamani ya shilingi Milioni 60 kwa kituo cha kulea watoto yatima cha Jeshi la Wokovu, Kurasini na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 08, 2024.
Msaada huo unajumuisha mahitaji mbalimbali kwa watoto yatima na vifaa tiba.
Wanawake hao pia wameshiriki katika zoezi la uchunguzi wa saratani ya matiti na mlango wa kizazi katika Kituo cha Afya cha TPA, zoezi linaloratibiwa na kituo hicho pamoja na Chama cha Madaktari Wanawake Tanzania ( MEWATA).