Wanaume fuatilieni afya zenu kama mnavyofuatilia mpira

0
287

Naibu Waziri wa TAMISEMI (Afya), Dkt. Festo Dugange amewakumbusha wananume kufuatilia afya zao na afya za watoto kama wanavyofuatilia mechi za mataifa ya Afrika (AFCON 2023) nchini Ivory Coast.

Dkt. Dugange ameitoa kauli hiyo katika uwanja wa Mbagala Zakhem mkoani Dar Es Salaam wakati akizundua zoezi la uchunguzi wa afya na chanjo kwa wananchi wa mkoa huo zoezi lilillowakutanisha wananchi kutazama mechi ya Tanzania na Morocco.

“Tunamwamko mkubwa katika kufuatilia michezo hususani AFCON2023, tunapenda sasa mwamko huo akinababa wenzangu kujali na kulinda afya kinga kwa watoto maana akinamama wametuzidi mbali juu ya afya ya watoto wetu na kuzingatia afya zao wenyewe,” amesema Dkt. Dugange