Wanasiasa waaswa kutunza Amani

0
280

Wanasiasa nchini wameaswa kuyatumia majukwaa ya kisiasa kunadi sera zao na si kuchafuana, ili kudumisha amani na utulivu uliopo nchini.

Wakizungumza wakati wa kongamano la kuliombea Taifa amani wakati huu wa kuelekea kwenye uchaguzi mkuu, viongozi wa dini katika Kata ya Igogo jijini Mwanza wamewahimiza wanasiasa kuchunga ndimi zao ili kuiwezesha Tanzania kuendelea kuwa kisiwa cha amani.

Wadau mbalimbali wakiwemo wazee wa Chama Clcha Mapinduzi (CCM) pamoja na viongozi wa dini katika kata hiyo wameweka mikakati ya kuimarisha amani na utulivu ikiwemo kuliombea taifa.

Mikakati hiyo inalenga kuhakikisha amani inatawala kabla, wakati na baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.

Afisa Mtendaji wa Kata ya Igogo, Benedicto Kabadi amewaondoa hofu wakazi wa kata hiyo kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vitahakikisha utulivu unakuwepo wakati wote.