Jopo la Wanasheria na viongozi wa serikali ya Tanzania, wakiwa nje ya mahakama ya Gauteng ya nchini Afrika Kusini, kufuatilia hatma ya kushikiliwa kwa ndege aina ya Airbus 220 – 300, mali ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) inayoshikiliwa kwa amri ya Mahakama.
Wanasheria pamoja na viongozi hao wanaongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Masharìki Dkt Damas Ndumbaro ambaye pia ni Wakili.