Wanaotuhumiwa kuchakachua mbolea kizimbani

0
266

Watuhumiwa wawili wa sakata la uchakachuaji wa mbolea ya ruzuku mkoani Njombe na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi Milioni 26, wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mkoa huo kwa kosa la uhujumu uchumi.

Pamoja na shtaka hilo kuu, watuhumiwa hao pia wanakabiliwa na mashtaka mengine matatu yakiwemo ya uuzaji wa mbolea feki, kula njama ya kutenda kosa na kuisababishia hasara Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA).