Wanaopitiwa na LTIP kupata hati

0
190

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhandisi Anthony Sanga amesema wizara hiyo itahakikisha inatoa Hati Miliki za Ardhi katika maeneo yote ambayo mradi wa Uboreshaji Usalama wa Milki za Ardhi (LTIP) unatekelezwa.

Mhandisi Sanga amesema hayo wilayani Nzega mkoani Tabora wakati wa ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu ya Serikali (PAC), ilipokwenda kukagua hatua iliyofikiwa na thamani ya fedha iliyotumika katika utekelezaji wa mradi wa LTIP kwenye halmashauri ya Mji wa Nzega.

Mhandisi Sanga ametoa kauli hiyo baada ya baadhi ya wajumbe wa PAC kutaka utekelezaji mradi wa LTIP unaoendelea katika maeneo mbalimbali nchini uende pamoja na utoaji hati miliki za ardhi.

‘’Wananchi wa Nzega tuwahakikishie sisi kama wizara tutahakikisha muda tuliokusudia kukamilisha mradi basi hati mnapata. Wote mtazipata hati na utoaji wa hati ni hatua ya mwisho,’’ Amesema Mhandisi Sanga.