Wanaonyanyasa walimu Njombe waonywa

0
137

Mkuu wa mkoa wa Njombe, Antony Mtaka amewataka baadhi ya viongozi wa ngazi za halmashauri na mkoa wanaowanyanyasa walimu kwa kuwatolea lugha siziso na staha pindi wanapofika kuwasilisha changamoto zao kuacha tabia hiyo mara moja.

Mtaka amesema, amekuwa shuhuda wa visa kadhaa ambavyo walimu wamekuwa wakifanyiwa na baadhi ya maafisa elimu, maafisa utumishi, waratibu elimu na walimu wakuu, na kuongeza kuwa yeyote atakayebainika akimtolea lugha zisizo rafiki mwalimu atachukuliwa hatua stahiki.

Mtaka ametoa onyo hilo wakati wa kufunga kikao kazi cha tathmini ya ubora wa elimu mkoani Njombe.

Mtaka amesema kwa kipindi atakachokuwa Njombe atahakikisha anafanya mageuzi makubwa katika sekta ya elimu, Ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mkoa huo unaongoza kitaifa katika mitihani yote ya Taifa ya kidato cha nne, kidato cha sita na darasa la nne.